Thursday, May 5, 2016

Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza

*Tanzania.* *TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI* Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza. Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo


mage: Profesa-Msanjila] *Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Z

.

Tuesday, December 24, 2013

VIFAHAMU VIVUTIO VILIVYOKO MKOA WA RUVUMA VYENYE MANDHARI YA KUVUTIA

Ndugu msomaji wa Blog hii Tanzania ni Nchi tajiri kwa kuwa na Vivutio na mandhari yenye mvuto wa aina yake ambayo wageni huitamani na kuwaacha wazawa wakishindwa kuithamini eidha kwa kutojua umuhimu wake au kwa kuwa hafahamu faida ama kama inamnufaisha. Picha hiyo ni Maporomoko ya Maji yaliyopo Chipole nje kidogo ya Mji wa Songea ambayo husaidia upatikanaji wa maji kwa ukanda unaozunguka eneo hilo aliyesimama katika maporomoko hayo ni Mgeni Muethiopia Mr Doglas alipotembelea na kufurahia hali hiyo ambayo kwao ni nadra kuiona. Je wazawa tunajifunza nini?
 Maji ya Kuvutia unayoyaona ni Maji yanayopatikana katika Ziwa Nyasa lililopo Tanzania na Nchi Jirani ya Malawi huo ni upande wa Tanzania na jiwe linaloonekana ni kivutio cha aina yake ambalo lina Pango kubwa kwa Nyuma lenye uwezo wa kuhifadhi watu zaidi ya 200 pango hilo lilitumika wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia ambapo wananchi wajificha katika pango hilo na huo mti ulio pembeni umeshikiliwa na Mawe tu haujafika ardhini cha ajabu ni kwamba una umri wa zaidi ya karne moja.
 Mawandishi wa Blog hii Bi Judith Lugoye alipotembelea Ziwa hilo kufahamu utalii uliopo Ziwa Nyasa na akifanya kazi ya kurekodi mandhari nzuri ya Ziwa Nyasa.


 Hapo ni Nyuma ya Jiwe la Pomonda ambapo mwandishi amesimama akielekea kwenye Pango la Pomonda kuona umuhimu wa utalii katika kuhamasisha wananchi wazawa kuona umuhimu wa kuvitangaza vivutio hivyo. Kisiwa hicho cha Pomonda kinapatikana km 20 toka Nchi kavu ni mwendo wa dk 30 kwa mtumbwi, na bei ya utalii kufika kisiwa kilipo ni ndogo kabisa.
 Maji ya Ziwa Nyasa yakionekana kwa mvuto yenye rangi nzuri na kule mbele ni eneo la Kisiwa cha Pomonda kilichopo Liuli Wilaya ya Nyasa, jiwe hilo linaonekana ndilo lenye pango lenye uwezo wa aina yake.
 Hiyo ni hali ya Sun Light katika Ziwa Nyasa Mkoa wa Ruvuma majira ya Jioni.
 Hapo ni ndani ya Pango la Pomonda tukiwa tumetembelea na kustarehe bila wasiwasi pembeni ni baadhi ya waandishishi wakiwa wamechoka na mwendo wa kupanda vilima kukifikia kisiwa hicho.
Pamoja na Rasilimali na vivutio vingi vilivyopo katika wilaya hiyo mpya ya Nyasa hayo ni baadhi ya Makazi ya wananchi wa Wilaya hiyo, hicho ni Kijiji cha Nindi ambacho wakazi wake wanadai hawajawahi kumuona kiongozi yeyote akiwatembelea wala kupata Bendera yeyote ya taifa na nyinginezo pamoja na kufahamu wamepata Uhuru. Jee Falsafa ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania inaenda sambamba na yaliyopo?